Monday, May 20, 2013

KAMA WEWE NI MMOJA WA WANAOTARAJIA KUFANYA MTIHANI WA FORM SIXT MWAKAN YAANI 2014 TANGAZO HILI LINAKUHUSU


Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi, Mei 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kitaanza rasmi tarehe 1 Julai, 2013 kwa ada ya Shilingi 35,000/=. Kipindi cha malipo bila adhabu kitaishia tarehe 31 Agosti, 2013. Kuanzia tarehe 1 Septemba, 2013 hadi tarehe 30 Septemba, 2013 waombaji watajisajili kwa ada ya Shilingi 50,000/- (ada pamoja na faini).
Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti: http://www.necta.go.tz/ ya Baraza la Mitihani la Tanzania. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) watakazotumia kujisajili. Hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kupata namba rejea kutoka katika kituo anachokusudia kufanyia Mtihani. Wakuu wote wa vituo nchini watakabidhiwa namba rejea hizo kabla ya muda wa usajili kuanza na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...