Friday, May 10, 2013

BAADA YA SAKATA LA MGOMO WA DALADA IRINGA HAYA NDIYO MAJIBU YA SUMATRA


SAKATA LA MGOMO WA DALADALA IRINGA ,OFISA WA SUMATRA IRINGA MAJI YA SHINGO.....LIVE

 Mmoja kati ya  viongozi  wa madereva daladala  akiwatuliza madereva hao 

Ofisa  wa  Sumatra  mkoa  wa Iringa Rahim Kondo akisikilizia jazba za madereva daladala mjini Iringa ambao  wamemtaka kabla ya  kuanza  kikao  kuwaomba radhi kwa  kuwaita  wao ni  wafanyakazi  wa ndani na kamwe hataongea nao  zaidi ya  kuwapiga faini kubwa
Risti ambazo  wanadai  kuwa  wamekuwa  wakitozwa faini kubwa ambazo kisheria haipo kabisa

Hali  ya  mgomo  wa  madereva  daladala katika Manispaa ya  Iringa  limechukua  sura  mpya baada ya madereva  hao kuamua kueleza uozo uliopo katika ofisi  za Sumatra mkoa  wa Iringa  kuwa amekuwa chanzo cha  wao  kunyanyasika.

Madereva hao wamesema kuwa hawajapendezwa na utendaji kazi wa Sumatra ikiwa ni pamoja na kuondoka mkoa  wa Iringa kutokana na kushindwa  kuifanya kazi  hiyo kwa misingi inayokusudiwa.

Madereva  hao  wametoa kilio  chao katika  kikao cha kamati ya usalama barabarani  kilichofanyika katika ukumbi  wa  jumba la maendeleo mjini Iringa.

Kwani  wamedai kuwa vikwazo mbali mbali ambazo  wamekuwa  wakivipata  madereva mjini Iringa vinasababishwa na utendaji mbovu  wa Sumatra  mkoa  wa Iringa pamoja na baadhi ya  askari wa usalama barabarani  mkoa  wa Iringa ambao  wamekuwa  wakichangia  kuwakandamiza  zaidi.

Suala la kufutwa kwa  stendi ya posta na miyomboni kutakiwa  kupita badala ya  kuegesha daladala zao  pia  limekuwa ni kikwazo  zaidi kwa madereva hao na kuwa hawapo tayari  kuendelea  kufanya kazi iwapo  kiongozi  huyo wa Sumatra  mkoa  wa Iringa ataendelea  kuwepo ofisini .

Awali  mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani  mkoa  wa Iringa  Salim Abri Asas  aliwataka  madereva  hao kutuliza jazba na kueleza madai yao katika kamati  hiyo ili kuyatafutia ufumbuzi  wa  kudumu.

No comments:

Post a Comment

sikiliza ngoma zinazo kamata kwa sasa

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...